MZUNGUKO WA UKANUSHI WA JESPERSEN KATIKA LUGHA YA KISWAHILI
DOI:
https://doi.org/10.2023/hn35p166Abstract
Mzunguko wa Ukanushi wa Jespersen ni mfuatano wa michakato katika Isimu Historia ambao huelezea maendeleo ya kihistoria ya ukanushi katika lugha mbalimbali unaojenga mzunguko. Kwa kuwa Mzunguko wa Ukanushi wa Jespersen (MUJ) bado haujatazamwa katika lugha ya Kiswahili, makala haya yanakusudia kuziba pengo hilo. Makala haya ni matokeo ya uchambuzi wa mapitio ya maandiko mbalimbali yahusuyo ukanushi. Baadhi ya mifano ya tungo za ukanushi ni kutoka kwa mwandishi kutokana na tajiriba na utaalamu alionao katika isimu ya lugha ya Kiswahili na Kiingereza. Tajiriba hii inatokana na ufundishaji wa kozi za mofolojia na fonolojia kwa takribani miaka sita. Moja ya mapitio ya msingi ni Ashton (1944) japo yeye na wengine waliomfuata hawakugusia suala la MUJ. Makala haya yamebainisha kuwa katika lugha ya Kiswahili, MUJ ni vigumu kubainishwa kihistoria/kidaikronia kama ilivyobainishwa na Jespersen. Akitumia mfano wa lugha ya Kifaransa, kabla ya lugha hiyo haijasanifishwa kulikuwa na umbo moja la ukanushi ne lililokuwa likijitokeza kabla ya kitenzi, baada ya lugha hiyo kusanifishwa; umbo lingne la ukanushi pas liliongezeka mwishoni mwa kitenzi na baadaye Kifaransa cha mitaani kiliibuka huku kikipuuza kutumia kikanushi ne, hivyo, kurudi tena katika mfumo wa ukanushi wa mwanzo wa tungo kuwa na kikanushi kimoja. Mtiririko huu ulionekana kujenga hali ya mzunguko/uduara. Makala haya yamebainisha kwamba suala hilo katika Kiswahili hujitokeza kisinkronia kwa kuutazama ukanushi kwa jinsi ulivyo kwa wakati wa sasa (kipindi hiki cha miaka ya 2000) katika Kiswahili. MUJ katika Kiswahili hujitokeza katika misingi kwamba baadhi ya vitenzi vina umbo moja la ukanushi wakati vitenzi vingine vina maumbo mawili. Kimantiki, tungo hizo zenye maumbo mawili ya ukanushi zinaonesha kuwa na dhana ya maana ya ukanushi moja na siyo mbili ndani ya kitenzi kimoja. Kwa hivyo, vinaleta hali ya mzunguko kwa maana ya kwamba kumekuwa na ongezeko la kikanushi cha pili lakini dhana ya maana ya ukanushi imerudi kuwa moja sawa na vitenzi vyenye kikanushi kimoja.
Downloads
Published
Issue
Section
License
Copyright (c) 2025 JARIDA LA CHAUKIDU

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial 4.0 International License.
License Terms Under CC Attribution-NonCommercial 4.0 (CC BY-NC 4.0)
1. Scope of Use
- Readers who purchase access to the journal articles are permitted to:
- Read: Access and view the content for personal use.
- Share: Share the purchased article in limited, non-commercial ways (e.g., with colleagues for educational or research purposes).
- Adapt: Create derivative works (e.g., summaries or adaptations) for non-commercial purposes.
2. Conditions of Use
- Attribution:
- Proper credit must be given to the author(s) and the journal when sharing or adapting content.
- Attribution must include the author(s)’ names, the article title, journal name, volume/issue, and a link to the journal or article DOI.
- Changes made to the work must be clearly indicated and properly attributed.
- NonCommercial:
- Articles may not be used for commercial purposes, including but not limited to resale, redistribution for financial gain, or inclusion in commercial products or services.
- Institutional use (e.g., for training or workshops) must comply with non-commercial terms unless explicit permission is granted by the journal.
3. Access and Sharing Restrictions
- Paid Access: Access to the journal articles is limited to subscribers or individuals who purchase the articles. Unauthorized distribution or sharing of the full article is prohibited.
- No Additional Restrictions: Readers may not apply further legal or technical restrictions that limit others from using the content as allowed by this license.
4. Prohibited Uses
- Articles may not be:
- Distributed on commercial platforms without explicit permission.
- Used in any activity that generates direct or indirect monetary profit (e.g., as part of paid courses or events) without prior approval from the journal.
- Modified for purposes that could misrepresent the original intent of the work.
5. Disclaimer
- The content is provided “as is,” without any guarantees or warranties from the authors or the journal.
- Neither the authors nor the journal accept liability for any claims, damages, or issues arising from the use of the article.
6. Additional Notes
- For Readers: Purchased content is for personal, educational, or research use only, subject to the non-commercial and attribution conditions.
- For Institutions: Institutions purchasing bulk access or subscriptions must ensure that access is limited to registered users and complies with non-commercial use conditions.
For the full legal text of the CC BY-NC 4.0 license, visit:
https://creativecommons.org/licenses/by-nc/4.0/legalcode