MWINGILIANOMATINI KATIKA USAWIRI WA MWANAMKE KATI YA TAMTHILIA ZA KILIO CHA HAKI YA A. MAZRUI NA KIGOGO YA P. KEA

Authors

  • Justus Kyalo Muusya Author
  • Leah W. Mwangi Author

DOI:

https://doi.org/10.2023/3vqkv634

Abstract

Mwingilianomatini ni hali ya kazi mbili au zaidi za fasihi kuingiliana. Mwingiliano huu waweza kutokea kisadfa ama waweza kuwa umetokea ili kutimiza matakwa fulani ya mtunzi. Mwingilianomatini huweza kutokea katika vipengele mbalimbali vya kazi zinazohusika hususan katika: muundo, msuko, uumbaji wa wahusika na uhusika, mtindo, masuala yanayoshughulikiwa miongoni mwa mambo mengine. Makala haya yanalenga kujadili hali ya kuingiliana inayojitokeza kati ya tamthilia ya Kilio cha Haki (A. Mazrui) na Kigogo (P. Kea). Utafiti awali unaonesha kuwa tamthilia hizi mbili zinaingiliana katika vipengele vingi mathalani: usawiri wa wahusika na uhusika, muundo, na msuko wa vitushi kati ya mambo mengine. Hata hivyo, uchunguzi utajikita zaidi katika kutalii suala la usawiri wa mwanamke. Lengo la makala haya ni kutathmini mwingiliano uliopo kati ya tamthilia hizi mbili ili kufafanua namna tamthilia hizi zinavyojengana na kukamilishana katika kusawiri masuala ya jinsia ya kike. Je, kuna mwingilianomatini katika kusawiri masuala ya wanawake katika tamthilia ya Kigogo na ile ya Kilio cha Haki? Kazi hizi mbili zimechanganuliwa kwa mwongozo wa mihimili ya Nadharia ya Mwingilianomatini.

Downloads

Download data is not yet available.

Published

2025-01-22

How to Cite

Muusya, J. K., & Mwangi, L. W. (2025). MWINGILIANOMATINI KATIKA USAWIRI WA MWANAMKE KATI YA TAMTHILIA ZA KILIO CHA HAKI YA A. MAZRUI NA KIGOGO YA P. KEA. JARIDA LA CHAUKIDU, 161-173. https://doi.org/10.2023/3vqkv634