UCHANGANUZI WA MWINGILIANO WA MANENO KATIKA MAZUNGUMZO KWA KISWAHILI MIONGONI MWA WANAFUNZI WA SHULE YA UPILI UGANDA

Authors

  • Mulei Martin Author

DOI:

https://doi.org/10.2023/ayp4tf42

Abstract

Lugha huingiliana na kuathiriana zaidi zinapotumiwa katika mazungumzo katika eneo mahususi la kijiografia. Mwingiliano wa lugha hujitokea katika viwango anuwai vya kiisimu mojawapo ikiwa mwingiliano wa maneno kati ya L1 na L2. Makala haya yameshughulikia matokeo ya utafiti kuhusu uchanganuzi wa mwingiliano wa maneno katika mazungumzo kwa Kiswahili kati ya lugha ya Kigisu na Kiswahili nchini Uganda. Utafiti huu ulitokana na tafiti za hapo awali zinazoripoti kwamba lugha ya kwanza huathiri umilisi wa lugha ya pili katika nyanja mbalimbali za kiisimu. Kwa hiyo, makala haya yanaripoti kuhusu matokeo ya matumizi ya maneno ya vitenzi na nomino miongoni mwa wanafunzi wanaojifunza na kuzungumza Kiswahili kama lugha ya pili ili kubainisha jinsi lugha ya Kigisu inavyoathiri lugha ya mazungumzo kwa Kiswahili miongoni mwa wanafunzi wa shule za upili kama lugha ya pili. Nadharia za Mwingiliano Lugha ya Selinker (1972), na Uchanganuzi Makosa kama inavyoelezwa na Lennon (2008) zilitumika kubainisha athari za mwingiliano wa maneno kati ya L1 na L2. Data ilikusanywa kutoka kwa wanafunzi 78 wa kidato cha tatu miongoni mwa wanafunzi wa shule nne za upili wanaoongea Kigisu kama L1 na ambao ni wanafunzi wa lugha ya Kiswahili. Matokea ya utafiti yanadhihirisha ujumuishaji wa nomino na vitenzi katika mazungumzo kwa Kiswahili, uhamishaji wa nomino na vitenzi kutoka L1 kwa L2 na ubadilishanaji wa nomino na vitenzi vya Kiswahili na vile vya Kigisu katika mazungumzo.

Downloads

Download data is not yet available.

Published

2025-01-22

How to Cite

Martin, M. (2025). UCHANGANUZI WA MWINGILIANO WA MANENO KATIKA MAZUNGUMZO KWA KISWAHILI MIONGONI MWA WANAFUNZI WA SHULE YA UPILI UGANDA. JARIDA LA CHAUKIDU, 246-258. https://doi.org/10.2023/ayp4tf42