UNAFIKI WA VIONGOZI WA KISIASA KAMA MKAKATI WA KUWAWEKA MAMLAKANI: MFANO KUTOKA RIWAYA ZA KATAMA MKANGI: MAFUTA NA WALENISI

Authors

  • Naomi Musembi Author

DOI:

https://doi.org/10.2023/7ykkej30

Abstract

Makala haya yanaangazia usawiri wa unafiki wa viongozi wa kisiasa kama mkakati wa kuwaweka mamlakani katika riwaya za Katama Mkangi Mafuta na Walenisi. Riwaya zote mbili ni za kiitikadi. Zinachunguza jinsi mfumo wa kisiasa unaodhibitiwa na tabaka la wachache unavyoweza kuathiri maisha ya wanaotawaliwa kisiasa. Riwaya hizi zinaonesha uovu uliopo katika tawala ambazo hazitilii maanani masilahi ya wanyonge. Ni kielelezo cha jinsi jamii inavyoweza kujinasua kutoka katika mfumo unaowakandamiza na unaowadhalilisha wengi. Mkangi amesawiri viongozi dhalimu wa kibepari wanaojiweka na kujisetiri mamlakani kupitia unafiki. Makala haya yanadhamiria kusawiri madhila wanayotendewa wanajamii na viongozi dhalimu wasiowajali kupitia unafiki ambao wameufanya kuwa ukweli. Kilele cha uozo wa viongozi wa kisiasa kinajitokeza wakati ambapo uhuru wa kuongea unadhibitiwa na yeyote anayepatikana na ‘hatia’ hii anahukumiwa kifo au anapata adhabu ya kufutwa kazi pasipo na sababu yenye mashiko. Jitihada za wanyonge za kukata silisili za udhalimu zinabainika wanapoamua kupindua mfumo huu wa kisiasa kwa kuwatimua viongozi dhalimu na wanafiki kupitia mapinduzi. Umuhimu wa makala haya ni kubainisha kuwa kupitia kazi za sanaa, hasa fasihi andishi, msomaji anaweza kubaini hali halisi ya maisha yake na wakati huohuo kupata suluhu ya kutatua matatizo yanayomkumba na jamii yake.

Downloads

Download data is not yet available.

Published

2025-01-22

How to Cite

Musembi, N. (2025). UNAFIKI WA VIONGOZI WA KISIASA KAMA MKAKATI WA KUWAWEKA MAMLAKANI: MFANO KUTOKA RIWAYA ZA KATAMA MKANGI: MAFUTA NA WALENISI. JARIDA LA CHAUKIDU, 268-291. https://doi.org/10.2023/7ykkej30