MATUMIZI YA FASIHI SIMULIZI KATIKA KAMPENI ZA UCHAGUZI TANZANIA

TATHMINI YA DHIMA YA NYIMBO

Authors

  • Fokas Nchimbi Author

DOI:

https://doi.org/10.2023/g837nb36

Abstract

Fasihi simulizi kama chombo cha kazi cha jamii haiwezi kujitenga na jamii katika shughuli zake kama vile za kiuchumi, kiutamaduni, kijamii, na kisiasa. Makala haya yanaeleza matumizi ya fasihi simulizi katika kampeni za siasa nchini Tanzania kwa kutumia kipengele cha nyimbo. Makala yanaeleza kuwa nyimbo ni nyenzo mojawapo inayotumika katika michakato ya kisiasa ikiwa ni pamoja na mikutano ya kampeni za uchaguzi. Data za makala haya zinazotokana na nyimbo za kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 zilizotumika kueleza falsafa, sera, dira, na matarajio ya wanasiasa katika ugombea wao wa nafasi za uongozi wa kisiasa. Kwa kutumia Nadharia ya Uhalisia wa Urasimi, makala haya yanaonesha kuwa nyimbo za kampeni za uchaguzi zinatumika kueleza ukweli wa mambo bila kutia chuku. Nyimbo hizi ziznaeleza mambo dhahiri ya kila siku na yanayoweza kuthibitika. Makala haya yanaeleza kuwa mbinu ya matumizi ya nyimbo katika kampeni za kisiasa za Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, na bila shaka katika kampeni zilizotangulia na zile zitakazokuja baadaye, ilitumika kipragmatiki kwa minajili ya kufikia matarajio ya kisiasa ya makundi ya wanasiasa na vyama vya siasa kwa ujumla. Kwa upande mmoja, mbinu hiyo ilikuwa na lengo la kutengeneza hadhara za wapiga kura na kuiweka tayari kwa ajili ya kusikiliza kampeni na hatimaye baadaye kupiga kura. Hali kadhalika, ilikuwa na azma ya kueleza na kusifu sera na falsafa za wagombea na vyama vyao vya siasa. Vilevile, ilikuwa ni mbinu ya kupinga sera na falsafa ya wagombea na vyama vingine. Katika makala haya, inaelezwa kuwa, pamoja na malengo hayo, lengo kuu kupita yote la kutumia mbinu ya nyimbo, kama kipengele cha fasihi simulizi, ilikuwa hatimaye kupata ushindi katika uchaguzi wenyewe.

Downloads

Download data is not yet available.

Published

2025-01-22

How to Cite

Nchimbi, F. (2025). MATUMIZI YA FASIHI SIMULIZI KATIKA KAMPENI ZA UCHAGUZI TANZANIA: TATHMINI YA DHIMA YA NYIMBO. JARIDA LA CHAUKIDU, 110-120. https://doi.org/10.2023/g837nb36