Abstract
Makala haya yanaangazia matumizi ya lugha katika riwaya inayosadikiwa kuwa ya kwanza ya Kiswahili ya Uhuru wa Watumwa (1934) iliyoandikwa na James Mbotela na riwaya ya kwanza ya Kiswahili ya majaribio ya Nagona (1990) ya Euphrase Kezilahabi, iliyoandikwa takribani miaka hamsini baadaye. Makala yanajadili matumizi ya lugha ya Kiswahili kwa kuangalia tofauti za matumizi yake katika riwaya hizo mbili za Kiswahili, vikiwamo vipengele kama vile vya uteuzi wa msamiati, lugha ya usimulizi, lugha ya majigambo, lugha ya ucheshi na kadhalika. Pia, makala yanajadili jinsi ambavyo riwaya hubadilika ikiendana na mabadiliko yanayoendelea kutokea katika jamii.

This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.
Copyright (c) 2025 Jarida la CHAUKIDU
