HADHI YA TONI YA KIKINGA

Waandishi

  • Sebastian Nyerere Mbwillow ##default.groups.name.author##

DOI:

https://doi.org/10.2023/kwp3cx44

Muhtasari

Tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa lugha ya Kikinga ni miongoni mwa lugha zilizotokana na lugha azali ya Mame-Bantu huku zikikubaliana kwamba lugha ya Kikinga ina toni (taz. Johnston 1922; Guthrie, 1948 na Clements na Goldsmith, 1984). Schadeberg (1973) alifanya utafiti wa tabia za ujitokezaji wa toni katika lugha ya Kikinga kwenye vipengele vya nomino na njeo, kwa kutumia Kiunzi Rasmi cha Fonolojia Zalishi (KRFZ) (Chomsky na Halle, 1968). Katika utafiti wake, Schadeberg (ktj), aliona kwamba lugha ya Kikinga ina mfumo zuizi wa toni. Tabia za toni katika vipengele vingine vya aina za maneno hazikushughulikiwa. Hii inatoa uhitaji wa kufanyika utafiti mwingine wa tabia za toni katika aina nyingine za maneno ili kupata hitimisho madhubuti la tabia za toni katika lugha ya Kikinga.

Downloads

Download data is not yet available.

Imechapishwa

2025-01-22

Jinsi ya Kunukuu

Mbwillow, S. N. (2025). HADHI YA TONI YA KIKINGA. JARIDA LA CHAUKIDU, 198-205. https://doi.org/10.2023/kwp3cx44