TATHMINI YA MCHANGO WA VYOMBO VYA HABARI VYA KICHINA KATIKA KUKUZA NA KUENEZA KISWAHILI
DOI:
https://doi.org/10.2023/6cphhf70Muhtasari
Vyombo vya habari vya Kichina vimekuwapo katika eneo la Afrika Mashariki tangu miaka ya 1960. Redio China Kimataifa (CRI) ilianza matangazo yake kwa lugha ya Kiswahili nchini Tanzania mnamo Septemba 1961. Ili kupata wafanyakazi wa Kichina walio na uwezo wa Kiswahili, lugha ya Kiswahili ilianza kufundishwa kama somo katika Chuo cha Utangazaji cha Beijing. Hadi sasa idhaa ya Kiswahili ya CRI inatangaza katika lugha ya Kiswahili. Wasimamizi wengi wa idhaa hii ni Wachina na wanakimudu Kiswahili vilivyo. Katika miaka ya hivi karibuni, hususani kuanzia mwaka 2011, vyombo vya habari vya Kichina vinavyotangaza katika lugha ya Kiswahili vimeongezeka. Baadhi ya hivi vyombo ni Shirika la Habari la Xinhua (Kupitia runinga yake ya CNC mtandaoni), shirika la runinga la CCTV (mtandaoni) na kampuni ya usambazaji wa mawimbi ya StarTimes. Tangu ongezeko hili lishuhudiwe, hakujakuwapo na utafiti wa kuonesha ni kwa njia gani vyombo hivi vimechangia katika ukuzaji na uenezaji wa lugha ya Kiswahili. Makala hii ililenga kufafanua ni kwa njia gani vyombo vya habari vya Kichina vimechangia katika kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili. Ili kufanikisha lengo hili, mbinu mbalimbali za utafiti zilitumiwa. Makala mbalimbali zilisomwa na kuchanganuliwa kwa kina. Vilevile, vipindi na matangazo kadhaa yanayopeperushwa katika vyombo hivi yalichanganuliwa. Mwishowe, wafanyakazi wa baadhi ya vyombo hivi walihojiwa. Matokeo ya utafiti huu yaliwasilishwa kwa njia ya ufafanuzi.
Downloads
Imechapishwa
Toleo
Sehemu
Leseni
Hakimiliki (c) 2025 JARIDA LA CHAUKIDU

Kazi hii imewekwa chini ya Leseni ya Creative Commons Kutambulisha-Isiyo ya Kibiashara 4.0 Kimataifa.
Masharti ya Leseni Chini ya CC Attribution-NonCommercial 4.0 (CC BY-NC 4.0)
1. Wigo wa Matumizi
Wasomaji wanaonunua upatikanaji wa makala za jarida wanaruhusiwa kufanya yafuatayo:
- Kusoma: Kupata na kuona maudhui kwa matumizi ya kibinafsi.
- Kushiriki: Kusambaza makala zilizopatikana kwa njia zisizo za kibiashara, kwa mfano, na wenzako kwa madhumuni ya kielimu au utafiti.
- Kubadilisha: Kuunda kazi zitokanazo (kwa mfano, muhtasari au marekebisho) kwa madhumuni yasiyo ya kibiashara.
2. Masharti ya Matumizi
Utoaji wa Sifa:
- Utambuzi sahihi lazima zitolewe kwa mwandishi/wandishi na jarida wakati wa kusambaza au kubadilisha maudhui.
- Utambuzi unapaswa kujumuisha jina la mwandishi/wandishi, kichwa cha makala, jina la jarida, toleo/matoleo, na kiungo cha jarida au DOI ya makala.
- Mabadiliko yoyote yaliyofanywa kwa kazi lazima yaonyeshwe wazi na kufanyiwa utambuzi ipasavyo.
Kutotumika Kibiashara:
- Makala hayawezi kutumiwa kwa madhumuni ya kibiashara, ikiwa ni pamoja na lakini sio tu kuuza tena, kusambaza kwa faida, au kuingizwa kwenye bidhaa au huduma za kibiashara.
- Matumizi ya kitaasisi (kwa mfano, kwa mafunzo au warsha) lazima yaambatane na masharti yasiyo ya kibiashara isipokuwa ruhusa ya wazi imetolewa na jarida.
3. Vizuizi vya Upatikanaji na Kushiriki
- Upatikanaji wa Kulipia: Upatikanaji wa makala za jarida unahusiana tu na waliojisajili au watu binafsi waliolipia makala. Usambazaji au kushiriki makala kamili bila ruhusa unakatazwa.
- Hakuna Vizuizi vya Ziada: Wasomaji hawaruhusiwi kuongeza vikwazo vya kisheria au kiteknolojia ambavyo vinazuia wengine kutumia maudhui kama ilivyoainishwa na leseni hii.
4. Matumizi Yanayokatazwa
Makala hayawezi:
- Kusambazwa kwenye majukwaa ya kibiashara bila ruhusa ya wazi.
- Kutumika katika shughuli zinazozalisha faida ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja (kwa mfano, kama sehemu ya kozi au matukio ya kulipiwa) bila idhini ya awali kutoka kwa jarida.
- Kubadilishwa kwa madhumuni yanayoweza kupotosha maana ya awali ya kazi.
5. Kanusho
- Maudhui yametolewa “kama yalivyo,” bila dhamana au uhakikisho wowote kutoka kwa waandishi au jarida.
- Waandishi wala jarida hawatawajibika kwa madai yoyote, madhara, au matatizo yanayojitokeza kutokana na matumizi ya makala.
6. Maelezo ya Ziada
- Kwa Wasomaji: Maudhui yaliyonunuliwa ni kwa matumizi ya kibinafsi, kielimu, au ya utafiti pekee, kwa kuzingatia masharti yasiyo ya kibiashara na utoaji wa sifa.
- Kwa Taasisi: Taasisi zinazonunua upatikanaji wa pamoja au usajili lazima zihakikishe kuwa upatikanaji unahusiana tu na watumiaji waliosajiliwa na unazingatia masharti yasiyo ya kibiashara.
Kwa maandishi kamili ya leseni ya CC BY-NC 4.0, tembelea:
https://creativecommons.org/licenses/by-nc/4.0/legalcode