KAMISHENI YA KISWAHILI YA AFRIKA MASHARIKI NA HATIMA YA VISWAHILI SANIFU
DOI:
https://doi.org/10.2023/t4kw9y83Muhtasari
Makala haya yanahusu nafasi ya Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki (KAKAMA) ikiwa ni tumaini jipya katika kudhibiti Viswahili sanifu katika nchi za Afrika Mashariki. Makala haya ni matokeo ya utafiti wa maktabani uliohakiki maandiko mbalimbali. Hoja kuu ya makala haya ni kwamba wakati wa ukoloni kulikuwa na Kiswahili sanifu cha Afrika Mashariki ambacho hakipo katika Afrika Mashariki huru. Hii ni kwa sababu, baada ya uhuru, Kamati ya Lugha (Kiswahili) ya Afrika Mashariki ilisambaratika na huo ukawa mwanzo wa kuibuka na kukua kwa Viswahili sanifu vya kimaeneo. Kuundwa kwa BAKITA Tanzania Bara na BAKIZA kwa upande wa Zanzibar kuliimarisha launi za Kiswahili. Pia, kutungwa kwa kamusi za KKS, KKF na KTK kwa Tanzania, Zanzibar na Kenya mtawalia ni ushahidi wa kuimarika kwa Viswahili sanifu vya kimaeneo. Vichocheo vya kuinukia kwa Viswahili hivyo vinaweza kuwa vingi lakini mawanda ya kisiasa kama kipengele muhimu cha ikolojia ya lugha yana nafasi ya juu zaidi kuliko sababu kuntu za kitaaluma. Hitimisho la makala haya ni kwamba inafaa kuwe na usanifishaji mpya na endelevu wa Kiswahili ili kurejesha umoja wa lugha wa Afrika Mashariki uliokuwapo wakati wa ukoloni. Wito wa makala haya ni kwamba KAKAMA inapaswa kuchukua hatua zinazostahiki kusitisha ongezeko la Viswahili sanifu kwa madai ya uhuru wa jamii kutumia lugha itakavyo. Muhuri wa ithibati lazima urejeshwe kwa KAKAMA ili kuhakikisha kwamba msamiati, miundo na matumizi ya Kiswahili sanifu kwa jumla yanasawazishwa. Matumizi rasmi ya lugha kama vile katika elimu na utawala yanapaswa kuwa yale yaliyokubaliwa na watumiaji kwa vigezo vya pamoja.
Downloads
Imechapishwa
Toleo
Sehemu
Leseni
Hakimiliki (c) 2025 JARIDA LA CHAUKIDU

Kazi hii imewekwa chini ya Leseni ya Creative Commons Kutambulisha-Isiyo ya Kibiashara 4.0 Kimataifa.
Masharti ya Leseni Chini ya CC Attribution-NonCommercial 4.0 (CC BY-NC 4.0)
1. Wigo wa Matumizi
Wasomaji wanaonunua upatikanaji wa makala za jarida wanaruhusiwa kufanya yafuatayo:
- Kusoma: Kupata na kuona maudhui kwa matumizi ya kibinafsi.
- Kushiriki: Kusambaza makala zilizopatikana kwa njia zisizo za kibiashara, kwa mfano, na wenzako kwa madhumuni ya kielimu au utafiti.
- Kubadilisha: Kuunda kazi zitokanazo (kwa mfano, muhtasari au marekebisho) kwa madhumuni yasiyo ya kibiashara.
2. Masharti ya Matumizi
Utoaji wa Sifa:
- Utambuzi sahihi lazima zitolewe kwa mwandishi/wandishi na jarida wakati wa kusambaza au kubadilisha maudhui.
- Utambuzi unapaswa kujumuisha jina la mwandishi/wandishi, kichwa cha makala, jina la jarida, toleo/matoleo, na kiungo cha jarida au DOI ya makala.
- Mabadiliko yoyote yaliyofanywa kwa kazi lazima yaonyeshwe wazi na kufanyiwa utambuzi ipasavyo.
Kutotumika Kibiashara:
- Makala hayawezi kutumiwa kwa madhumuni ya kibiashara, ikiwa ni pamoja na lakini sio tu kuuza tena, kusambaza kwa faida, au kuingizwa kwenye bidhaa au huduma za kibiashara.
- Matumizi ya kitaasisi (kwa mfano, kwa mafunzo au warsha) lazima yaambatane na masharti yasiyo ya kibiashara isipokuwa ruhusa ya wazi imetolewa na jarida.
3. Vizuizi vya Upatikanaji na Kushiriki
- Upatikanaji wa Kulipia: Upatikanaji wa makala za jarida unahusiana tu na waliojisajili au watu binafsi waliolipia makala. Usambazaji au kushiriki makala kamili bila ruhusa unakatazwa.
- Hakuna Vizuizi vya Ziada: Wasomaji hawaruhusiwi kuongeza vikwazo vya kisheria au kiteknolojia ambavyo vinazuia wengine kutumia maudhui kama ilivyoainishwa na leseni hii.
4. Matumizi Yanayokatazwa
Makala hayawezi:
- Kusambazwa kwenye majukwaa ya kibiashara bila ruhusa ya wazi.
- Kutumika katika shughuli zinazozalisha faida ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja (kwa mfano, kama sehemu ya kozi au matukio ya kulipiwa) bila idhini ya awali kutoka kwa jarida.
- Kubadilishwa kwa madhumuni yanayoweza kupotosha maana ya awali ya kazi.
5. Kanusho
- Maudhui yametolewa “kama yalivyo,” bila dhamana au uhakikisho wowote kutoka kwa waandishi au jarida.
- Waandishi wala jarida hawatawajibika kwa madai yoyote, madhara, au matatizo yanayojitokeza kutokana na matumizi ya makala.
6. Maelezo ya Ziada
- Kwa Wasomaji: Maudhui yaliyonunuliwa ni kwa matumizi ya kibinafsi, kielimu, au ya utafiti pekee, kwa kuzingatia masharti yasiyo ya kibiashara na utoaji wa sifa.
- Kwa Taasisi: Taasisi zinazonunua upatikanaji wa pamoja au usajili lazima zihakikishe kuwa upatikanaji unahusiana tu na watumiaji waliosajiliwa na unazingatia masharti yasiyo ya kibiashara.
Kwa maandishi kamili ya leseni ya CC BY-NC 4.0, tembelea:
https://creativecommons.org/licenses/by-nc/4.0/legalcode