MABADILIKO YA KIJAMII NA USAWIRI WA MWANAMKE: UCHAMBUZI WA WIMBO WA TAARABU WA ISHA RAMADHANI.
UCHAMBUZI WA WIMBO WA TAARABU WA ISHA RAMADHANI
DOI:
https://doi.org/10.2023/px883t30Muhtasari
Kihistoria mwanamke katika jamii amekuwa ni chombo kilicho katika mabadiliko ya aina mbalimbali katika vipindi tofautitofauti. Mabadiliko hayo, hujitokeza takriban karne mpaka karne kulingana na mifumo ya jamii husika. Kwa mfano, yamejitokeza katika mfumo wa kijamaa, kimwinyi, kibepari kwa kutaja baadhi tu. Katika kila mfumo tunaona jinsi mwanamke anavyosawiriwa kupitia kazi mbalimbali za fasihi ya Kiswahili kuanzia kipindi cha utawala wa Waarabu wa Omani wakati wa ukoloni katika Afrika Mashariki mpaka kipindi tulichopo sasa. Wanawake katika jamii za Kiafrika, wanakumbana na changamoto za aina mbalimbali katika jamii zinazotawaliwa na wanaume. Hali hii imesababisha kuwapo kwa harakati za kumkomboa mwanamke dhidi ya mfumo kandamizi kutoka kwa mwanamume. Je, ukombozi huo umepatikana au la? Makala haya, yana lengo la kufafanua usawiri wa mwanamke katika karne hii ya ishirini na moja sambamba na kubainisha mambo yaliyosababisha kuwapo kwa mabadiliko hayo katika usawiri wa mwanamke. Mifano itatoka katika wimbo ulioimbwa na Isha Ramadhani unaoitwa ‘Mwanamke Mpango Mzima’. Pia, makala haya, yanachambua wimbo uliotungwa na kuimbwa na mwanamke ili kuweza kubaini mtazamo wa mwanamke mwenyewe juu ya wanawake wenzake wa jamii za Afrika Mashariki kwa ujumla.
Downloads
Imechapishwa
Toleo
Sehemu
Leseni
Hakimiliki (c) 2025 JARIDA LA CHAUKIDU

Kazi hii imewekwa chini ya Leseni ya Creative Commons Kutambulisha-Isiyo ya Kibiashara 4.0 Kimataifa.
Masharti ya Leseni Chini ya CC Attribution-NonCommercial 4.0 (CC BY-NC 4.0)
1. Wigo wa Matumizi
Wasomaji wanaonunua upatikanaji wa makala za jarida wanaruhusiwa kufanya yafuatayo:
- Kusoma: Kupata na kuona maudhui kwa matumizi ya kibinafsi.
- Kushiriki: Kusambaza makala zilizopatikana kwa njia zisizo za kibiashara, kwa mfano, na wenzako kwa madhumuni ya kielimu au utafiti.
- Kubadilisha: Kuunda kazi zitokanazo (kwa mfano, muhtasari au marekebisho) kwa madhumuni yasiyo ya kibiashara.
2. Masharti ya Matumizi
Utoaji wa Sifa:
- Utambuzi sahihi lazima zitolewe kwa mwandishi/wandishi na jarida wakati wa kusambaza au kubadilisha maudhui.
- Utambuzi unapaswa kujumuisha jina la mwandishi/wandishi, kichwa cha makala, jina la jarida, toleo/matoleo, na kiungo cha jarida au DOI ya makala.
- Mabadiliko yoyote yaliyofanywa kwa kazi lazima yaonyeshwe wazi na kufanyiwa utambuzi ipasavyo.
Kutotumika Kibiashara:
- Makala hayawezi kutumiwa kwa madhumuni ya kibiashara, ikiwa ni pamoja na lakini sio tu kuuza tena, kusambaza kwa faida, au kuingizwa kwenye bidhaa au huduma za kibiashara.
- Matumizi ya kitaasisi (kwa mfano, kwa mafunzo au warsha) lazima yaambatane na masharti yasiyo ya kibiashara isipokuwa ruhusa ya wazi imetolewa na jarida.
3. Vizuizi vya Upatikanaji na Kushiriki
- Upatikanaji wa Kulipia: Upatikanaji wa makala za jarida unahusiana tu na waliojisajili au watu binafsi waliolipia makala. Usambazaji au kushiriki makala kamili bila ruhusa unakatazwa.
- Hakuna Vizuizi vya Ziada: Wasomaji hawaruhusiwi kuongeza vikwazo vya kisheria au kiteknolojia ambavyo vinazuia wengine kutumia maudhui kama ilivyoainishwa na leseni hii.
4. Matumizi Yanayokatazwa
Makala hayawezi:
- Kusambazwa kwenye majukwaa ya kibiashara bila ruhusa ya wazi.
- Kutumika katika shughuli zinazozalisha faida ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja (kwa mfano, kama sehemu ya kozi au matukio ya kulipiwa) bila idhini ya awali kutoka kwa jarida.
- Kubadilishwa kwa madhumuni yanayoweza kupotosha maana ya awali ya kazi.
5. Kanusho
- Maudhui yametolewa “kama yalivyo,” bila dhamana au uhakikisho wowote kutoka kwa waandishi au jarida.
- Waandishi wala jarida hawatawajibika kwa madai yoyote, madhara, au matatizo yanayojitokeza kutokana na matumizi ya makala.
6. Maelezo ya Ziada
- Kwa Wasomaji: Maudhui yaliyonunuliwa ni kwa matumizi ya kibinafsi, kielimu, au ya utafiti pekee, kwa kuzingatia masharti yasiyo ya kibiashara na utoaji wa sifa.
- Kwa Taasisi: Taasisi zinazonunua upatikanaji wa pamoja au usajili lazima zihakikishe kuwa upatikanaji unahusiana tu na watumiaji waliosajiliwa na unazingatia masharti yasiyo ya kibiashara.
Kwa maandishi kamili ya leseni ya CC BY-NC 4.0, tembelea:
https://creativecommons.org/licenses/by-nc/4.0/legalcode