TAFSIRI BINAFSI KATIKA NADHARIA YA TAFSIRI: UTHABITI, CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO
DOI:
https://doi.org/10.2023/53532151Muhtasari
Nadharia ya tafsiri ni taaluma kongwe ulimwenguni ambayo imesaidia kukuza uchumi na maendeleo ya jamii kwa kurahisisha mawasiliano na kuunganisha ulimwengu. Tunapozungumzia tafsiri binafsi ni ile tafsiri inayofanywa na mwandishi wa matini chanzi kwa kuhawilisha mawazo ama ujumbe wa lugha chanzi kwenda lugha lengwa ambayo ni tofauti na ile aliyoitumia kuandikia matini ya awali. Swali la kujiuliza katika mchakato wa kutafsiri matini binafsi ni: je, mfasiri anatafsiri ama anahamisha mawazo yake aliyoyaandika kwa kutumia lugha chanzi na kuyaandika kwa kutumia lugha nyingine (lugha lengwa)? Je, ni mbinu zipi zinazotumika katika kutafsiri matini binafsi? Je, mfasiri binafsi hukumbana na changamoto zipi anapotafsiri matini yake? Kwa hiyo, makala haya inachunguza tafsiri binafsi katika nadharia ya tafsiri ili kubaini mbinu zinazotumika katika tafsiri binafsi, kubainisha changamoto za tafsiri binafsi na kutoa mapendekezo kuhusu tafsiri binafsi katika nadharia ya tafsiri. Ili kufikia malengo hayo, makala haya yametumia mifano ya matini mbili za fasihi, yaani riwaya ya Bwana Myombekere na Bibi Bugonoka Ntutalanalwo na Bulihwali (1980) iliyoandikwa na kutafsiriwa na Anicent Kitereza na tamthiliya ya Mtawa Mweusi (1970) ambayo ni tafsiri ya The Black Hermit (1968) tamthiliya iliyoandikwa na Ngugi wa Thiong’o na kisha kuitafsiri kwa lugha ya Kiswahili. Data za makala haya zilikusanywa kwa kutumia mbinu tatu, yaani mbinu ya usomaji wa machapisho, dodoso na usaili. Kwa kutumia Nadharia ya Ulinganifu, makala haya yanajadili kuwa tafsiri binafsi ni ile ambayo huzingatia nadharia na vitendo, kwa hiyo, mfasiri hukumbana na changamoto za kiisimu, kiutamaduni na kimaana katika mchakato wa tafsiri kama ilivyo katika tafsiri inayofanywa na mtu mwingine. Kwa hiyo, ujuzi wa lugha, utamaduni na nadharia za tafsiri ni mambo ya msingi katika kufanikisha mawasiliano ya kazi ya tafsiri bila kujali ni tafsiri binafsi au tafsiri inayofanywa na mtu mwingine.
Downloads
Imechapishwa
Toleo
Sehemu
Leseni
Hakimiliki (c) 2025 JARIDA LA CHAUKIDU

Kazi hii imewekwa chini ya Leseni ya Creative Commons Kutambulisha-Isiyo ya Kibiashara 4.0 Kimataifa.
Masharti ya Leseni Chini ya CC Attribution-NonCommercial 4.0 (CC BY-NC 4.0)
1. Wigo wa Matumizi
Wasomaji wanaonunua upatikanaji wa makala za jarida wanaruhusiwa kufanya yafuatayo:
- Kusoma: Kupata na kuona maudhui kwa matumizi ya kibinafsi.
- Kushiriki: Kusambaza makala zilizopatikana kwa njia zisizo za kibiashara, kwa mfano, na wenzako kwa madhumuni ya kielimu au utafiti.
- Kubadilisha: Kuunda kazi zitokanazo (kwa mfano, muhtasari au marekebisho) kwa madhumuni yasiyo ya kibiashara.
2. Masharti ya Matumizi
Utoaji wa Sifa:
- Utambuzi sahihi lazima zitolewe kwa mwandishi/wandishi na jarida wakati wa kusambaza au kubadilisha maudhui.
- Utambuzi unapaswa kujumuisha jina la mwandishi/wandishi, kichwa cha makala, jina la jarida, toleo/matoleo, na kiungo cha jarida au DOI ya makala.
- Mabadiliko yoyote yaliyofanywa kwa kazi lazima yaonyeshwe wazi na kufanyiwa utambuzi ipasavyo.
Kutotumika Kibiashara:
- Makala hayawezi kutumiwa kwa madhumuni ya kibiashara, ikiwa ni pamoja na lakini sio tu kuuza tena, kusambaza kwa faida, au kuingizwa kwenye bidhaa au huduma za kibiashara.
- Matumizi ya kitaasisi (kwa mfano, kwa mafunzo au warsha) lazima yaambatane na masharti yasiyo ya kibiashara isipokuwa ruhusa ya wazi imetolewa na jarida.
3. Vizuizi vya Upatikanaji na Kushiriki
- Upatikanaji wa Kulipia: Upatikanaji wa makala za jarida unahusiana tu na waliojisajili au watu binafsi waliolipia makala. Usambazaji au kushiriki makala kamili bila ruhusa unakatazwa.
- Hakuna Vizuizi vya Ziada: Wasomaji hawaruhusiwi kuongeza vikwazo vya kisheria au kiteknolojia ambavyo vinazuia wengine kutumia maudhui kama ilivyoainishwa na leseni hii.
4. Matumizi Yanayokatazwa
Makala hayawezi:
- Kusambazwa kwenye majukwaa ya kibiashara bila ruhusa ya wazi.
- Kutumika katika shughuli zinazozalisha faida ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja (kwa mfano, kama sehemu ya kozi au matukio ya kulipiwa) bila idhini ya awali kutoka kwa jarida.
- Kubadilishwa kwa madhumuni yanayoweza kupotosha maana ya awali ya kazi.
5. Kanusho
- Maudhui yametolewa “kama yalivyo,” bila dhamana au uhakikisho wowote kutoka kwa waandishi au jarida.
- Waandishi wala jarida hawatawajibika kwa madai yoyote, madhara, au matatizo yanayojitokeza kutokana na matumizi ya makala.
6. Maelezo ya Ziada
- Kwa Wasomaji: Maudhui yaliyonunuliwa ni kwa matumizi ya kibinafsi, kielimu, au ya utafiti pekee, kwa kuzingatia masharti yasiyo ya kibiashara na utoaji wa sifa.
- Kwa Taasisi: Taasisi zinazonunua upatikanaji wa pamoja au usajili lazima zihakikishe kuwa upatikanaji unahusiana tu na watumiaji waliosajiliwa na unazingatia masharti yasiyo ya kibiashara.
Kwa maandishi kamili ya leseni ya CC BY-NC 4.0, tembelea:
https://creativecommons.org/licenses/by-nc/4.0/legalcode