MITAZAMO YA LUGHA NA ELIMU KATIKA JAMII ZA AFRIKA MASHARIKI

Authors

  • Anne Jebet Author
  • Beatrice Mkenda Author

DOI:

https://doi.org/10.2023/hf8v8k13

Abstract

Nchi nyingi za Afrika Mashariki na barani Afrika zimejaliwa kuwa na idadi kubwa za lugha. Ni jambo la kawaida kukuta lugha zaidi ya mia moja zinazozungumzwa katika nchi moja pekee. Hali hii imeleta utata na hata kusababisha baadhi ya lugha kukosa wasemaji (Brock-Utne na wenzie, 2010). Kiswahili, lugha ya taifa nchini Kenya na Tanzania ni mojawapo ya lugha zinazokabiliwa na utata mkubwa hasa kuhusu matumizi yake kama lugha ya kufundishia au kufundishwa katika mifumo ya elimu. Huku wadau wengi wa lugha wakihimiza matumizi ya lugha itakayomwezesha mwanafunzi kujifunza na kuyaelewa mazingira yake, bado kuna athari kubwa katika kukabiliana na ulimwengu wa utandawazi. Makala haya yanakusudia kuchambua kwa undani zaidi mitazamo ya lugha katika Afrika ya Mashariki (nchi za Kenya na Tanzania) na kulinganua mitazamo ya lugha na umuhimu wake katika kupiga vita dhidi ya kasumba ya kikoloni na utumwa wa Kiingereza. Ingawa tafiti nyingi zimeeleza zaidi kuhusu sera za lugha katika nchi hizi, makala haya yanatoa hoja kuwa mitazamo ya lugha imeathiriwa sana na sera hizo za lugha na zaidi pia mambo mengine kama ubeberu wa kiisimu na utandawazi. Hivyo basi, tutachunguza jinsi makala na tafiti mbalimbali katika nchi hizi mbili, zilivyozungumzia masuala haya tangu wakati wa ukoloni hadi miaka ya karibuni na iwapo kumekuwa na mabadiliko yoyote.

Downloads

Download data is not yet available.

Published

2025-01-22

How to Cite

Jebet, A., & Mkenda, B. (2025). MITAZAMO YA LUGHA NA ELIMU KATIKA JAMII ZA AFRIKA MASHARIKI. JARIDA LA CHAUKIDU, 126-149. https://doi.org/10.2023/hf8v8k13

Most read articles by the same author(s)