DHIMA NA CHANGAMOTO ZA MATUMIZI YA TAFSIRI KATIKA UFUNDISHAJI WA KISWAHILI NCHINI UGANDA

Authors

  • Sarah Ndanu M. Ngesu Author
  • Leonard Muaka Author

DOI:

https://doi.org/10.2023/bak38m84

Abstract

Ufundishaji wa lugha ya kigeni au lugha ya pili kwa wanafunzi wenye umilisi wa lugha na desturi zao si jambo rahisi. Wakati mwingine, walimu hutumia tafsiri ili wanafunzi waweze kuelewa vipengele vya lugha ya kigeni inayofundishwa. Makala haya yanaangazia matumizi ya mbinu ya tafsiri katika shule za sekondari jijini Kampala nchini Uganda. Lengo la makala haya ni kujadili iwapo tafsiri inaweza kutambuliwa kama stadi ya tano katika ufundishaji wa Kiswahili kwa wageni. Utafiti huu umechochewa na mkanganyiko uliopo kuhusu nafasi ya tafsiri katika ufundishaji wa lugha. Ingawa tafsiri hutumiwa katika ufundishaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni, mbinu hii haibainishwi kama mbinu mojawapo ya ufundishaji kwenye mitaala. Data za utafiti ni za uwandani na maktabani. Data za uwandani zilikusanywa kwa njia ya ushuhudiaji, hojaji na uchambuzi wa nyaraka. Matokeo yanaonesha kwamba tafsiri ni mbinu inayotumiwa kwa upana katika ufundishaji wa Kiswahili nchini Uganda. Halikadhalika, makala haya yamebainisha kuwa Kiswahili ni lugha ya kigeni nchini Uganda, hali inayowafanya walimu kutegemea tafsiri baina ya Kiswahili na Kiingereza. Kwa kuhitimisha, makala haya yanashadidia kwamba hata kama tafsiri ina changamoto zake katika ufundishaji wa lugha za kigeni, haiwezi kukwepeka katika ufundishaji wa Kiswahili katika mazingira ambamo lugha hii haitumiwi katika mawasiliano ya kila siku.

Downloads

Download data is not yet available.

Published

2025-01-22

How to Cite

Ngesu, S. N. M., & Muaka, L. (2025). DHIMA NA CHANGAMOTO ZA MATUMIZI YA TAFSIRI KATIKA UFUNDISHAJI WA KISWAHILI NCHINI UGANDA. JARIDA LA CHAUKIDU, 87-109. https://doi.org/10.2023/bak38m84

Most read articles by the same author(s)